JNNK Programs

Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo ni nini?  

Ni muunganiko wa familia 10 - 15 zilipo karibu. JNNK isiwe kubwa sana kiasi kwamba wanajumuiya wakashindwa kujuana na kusaidiana kiroho na kimwili au isiwe ndogo sana hivyo kwamba hawawezi kujitegemeza kiuchumi, kueneza injili na kiutumishi. JNNK huwa ukoo wa Kristo, kwa kuwa kitu kimoja katika kuungana na Kristo Yesu (Gal. 3:27 - 28).

Parokia Teule ya Mt. Monica – Langoni Katika kutekeleza DIRA na DHIMA zake zipo taratibu mbali mbali zilizoanzishwa na kuratibiwa na Parokia Teule kwatika kuleta ufanisi na utendaji kazi bora katika Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo. Taratibu izo ni kama ifuatavyo;-


  • Sikukuu za Somo JNNK 
Kila jumuiya ni lazima iadhimishe kila mwaka sikukuu ya somo wao kwa Ibada ya Misa katika jumuiya yao. Sikukuu hii yaweza kuadhimishwa katika tarehe husika au kwa siku nyingine ifaayo. Kwa kufanya hivyo Umoja, Amani, Upendo na Mshikamano vitadumishwa na kudhihirishwa na wanajumuiya.
  • Mikutano ya JNNK na Kanda 
JNNK na Kanda zote kwa kushirikiana na Padre Mlezi zimeweka utatatibu maalumu wa wa kukutana kila mara moja kila mwezi ambapo viongozi wa kanda husika hujadiliana kuhusu maendeleo na changamoto zilizopo katika eneo lao mahalia na pale itakapowalazimu kwa ushauri au maelekezo watamshirikisha Padre mlezi. 
Huduma mbali mbali za kichungaji
  • Kutembelea JNNK 
Mapadre walezi wameweka utaratibu kwa kutembelea jumuiya zote katika kanda zote sita (6) kwa kufuata ratiba ilivyopangwa. Pia katika kuboresha na kuamsha Imani katoliki katika Parokia yetu Teule Mapadre na Viongozi wa JNNK wameweka utaraibu wa kutembelea Familia/Kaya moja moja wakiongozana na Viongozi wa jumuiya husika.
  • Wagonjwa na Wazee
Kanda na JNNK kwa Pamoja zimeweka utaratibu wa kutembelea wagonjwa na wazee katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kuwajulia hali kuwapa matumaini na misaada mbali mbali. Pia kwa kushirikiana na Kamati tendaji ya Parokia Teule wanabuni na kuweka taratibu mbali mbali za kupata misaada na ya hali na mali kwaajili ya kulisaidia kundi hili maaalumu na wale waliopo katika mazingira hatarishi.

  • Ibada za kanda 
Kila siku moja katika mwezi kutakuwepo na ibada ya Misa takatifu na mkutano wa wanajumuiya wote wa kanda, Watasali na kutatua matatizo yanayohusu Kanda yao. Na utaratibu ni kama ifuatavyo
  • Mazishi
JNNK na Kanda kwa kushirikiana na Padre mlezi  wameweka utarabu mzuri wa kufanya maziko ya wapendwa wetu kwa kuanzia kwenye ngazi ya jumuiya, na endapo kama aliyefariki alikuwa akiishi nje ya Parokia Teule, Jimbo au Mkoa ni wajibu wa wahusika kuleta barua kutoka kwa Paroko au Padre alipokuwa anaishi