Miradi ya Parokia Teule

Parokia Teule ya Mt. Monica Langoni ikijiandaa kuwa Parokia kamili na katika kujiimarisha kiimani/Kiroho na kiuchumi imeandaa, imekamilisha, na inatekeleza miradi mbali mbali kwa kushirikiana na waamini wake kama ifuatavyo

KIIMANI/KIROHO
Mafungo na Semina 
Viongozi wa JNNK na mashirika ya kitume hukutana na Padre Mlezi kila siku ya Ijumaa ya kwanza ya mwezi kwa kuabudu Ekarist takatifu, sala, tafakari na mengineyo.

Mashirika yote ya kitume kwa nyakati mbali mbali hupokea mafundisho na kutembelewa na Padre mlezi mara moja kila mwezi.

Waamini wote wa Parokia teule hujumuika kwenye mafungo na semina elekezi mbali mbali hapa parokiani kama vile Semina za kiroho katika Uinjilishaji wa kina, Semina za elimu ya Biblia, makongamano na nyingine nyingi. makongamano haya hufanyika hususani nyakati zifuatazo 
Kabla ya Pasaka, 
Katikati ya Mwaka, 
Kabla ya Noeli.

Kuboresha Duka la vitabu vya Dini Parokiani .

Kuaanda Makatekista bora na waadilifu wa Parokia.

Kuanzisha Mafunzo ya elimu ya Biblia na Muziki Mtakatifu.

Kuimarisha mwamko wa kusali katika Jumuiya pamoja na kuanzisha JNNK/seli za Watoto.

KIUCHUMI NA KIMAENDELEO
Ili tuweze kufikia lengo la kuwa Parokia kamili Parokia teule ya Mt. Monica Langoni inayo miradi mbali mbali ya kutekeleza na mingine imekwisha kukamilika

Makazi ya Mapadre 
Parokia teule kwa kushirikiana na waamini na wahisani imekamilisha ujenzi wa makazi ya kisasa kabisa ya mapdre, ambayo ni nyumba ya Ghorofa na ilizinduliwa na aliyekuwa Masimamizi wa kichungaji wa jimbo la Moshi Padre DEOGRATIAS MATIIKA mwaka 2019. 

Ujenzi wa Jiko la Makazi ya Mapadre na eneo la kufulia
Parokia Teule bado inaendelea na ujenzi wa jiko bora la kisasa lakuhudumia nyumba ya mapadre pamoja na eneo la kufulia na nyumba ya muhudumu.


Ujenzi wa Jengo la utawala
Parokia Teule sambamba na kuendelea na ujenzi wa jiko na sehemu ya kufulia pia tunaendelea na maboresho na ujenzi wa Jengo la kisasa la utawala lenye hadi ya parokia. 

Kusanifu Ujenzi wa Jengo jipya la kanisa.
Parokia Teule katika kiufanya uboreshwaji wa majengo yake yote, pia tunadhamiria kufanya usanifu wa ujenzi wa jengo jipya la kanisa litakaloendana na hadhi ya parokia yetu kabla ya kufika Dec 2022

Ununuzi wa Gari ya Parokia
Parokia Teule inaendelea kutafuta fedha na michango mbali mbali kutoka kwa waamini katika kufanikisha zoezi la Ununuzi wa gari maalumu la kisasa kwaajili ya parokia mpaka ifikapo 2021.

Ujenzi wa Shule ya Awali (Montessori)
Parokia Teule inadhamiria kuanza ujenzi wa shule ya awali ya parokia, ikiwa ni katika kusogeza huduma za kijamii karibu na waamini zoezi hili litamilika kabla ya kufika April 2022. 

Ujenzi wa Grotto ya Bikira Maria
Parokia Teule tunayofuraha kuwajulisha kwamba tumekamilisha ujenzi wa Grotto yetu ya Bikira Maria Msaada wa Kristo ambayo tulianza ujenzi wake  Dec. 2021.

Haya ni Maendeleo ya Ujenzi wa Grotto yetu ya Bikira Maria, Grotto ya kisasa inayojengwa kwa nguvu za waamini wa Parokia teule ya St. Monica Langoni

Kilimo cha kisasa cha Migomba na Bustani za Mboga
Parokia Teule pia kwa kutumia ardhi ya parokia inaendelea kufanya uboreshaji wa shamba la migomba na kuwa la kisasa, kadhalika kuboresha bustani za mboga pia.