Utaratibu wa Ibada Jumapili

Parokia Teule ya Mt. Monica Langoni imeweka utaratibu mzuri wa wa ibada siku ya jumapili kwa kuzingatia makundi mbali mbali, ikiwamo wazee, Vijana, Watu Wazima na Watoto. Utaribu huo ni kama ifuatavyo;-

MISA YA KWANZA
Hii ni Ibada Mahususi kwaajili ya watu wazima wenye ndoa na mafundisho na tafakari yake yanalenga katika Familia na ndoa. 

MISA YA PILI 
Hii ni Ibada mahususi kwaajili ya Vijana na Mafundisho yake na Tafakari yake yanalenga katika kumuunganisha kijana na Mungu na kutekeleza wajibu wake ili kutimiza wajibu wake kiroho, kimwili na kiuchumi.  

MISA YA TATU
Hii ni Ibada mahususi kwa ajili ya Watoto na mafundisho na tafaki yake yanalenga katika kuwaimarisha watoto katika kumjua Kristo na mafundisho yake yanalenga katika kujenga taifa la wachamungu na waadilifu.

MISA YA NNE
Hii ni Ibada Mahususi kwaajili ya watu wote waliokosa nafasi ya kuhudhuria ibada za asubuhi na wale waamini wa makundi maalumu  kama wazee na walemavu. Ibada hii mafundisho na tafakari yake ni mchanganyiko.
Pia kadiri ya mpangilio wa shughuli za kichungaji kabla ya adhimisho la Misa takatifu tunaanza na Baraka ya Sakramenti kuu saa 9:30 au saa 10:00 jioni