Huduma za Siku za Juma

Parokia Teule ya Mt. Monica Langoni inawathamini waamini wote na inawakaribisha sana Parokiani kwa ajili ya kuja kupata misaada mbali mbali ya kiofisi kwa siku zote za juma kuanzia jumatatu hadi ijumaa kwa utatibu ufuatao.


HUDUMA ZA SAKRAMENTI NDANI YA SIKU ZA JUMA
UBATIZO
Parokia Teule ya Mt. Monika inao utaratibu wa kutoa Sakramenti ya ubatizo kwa watoto wote siku ya Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi. Ikitanguliwa na semina kwa Wazazi/Walezi pamoja na wasimamizi.
Pia watoto hupata huduma hii wakati wa Pasaka ya pili.  Yani Jumatatu ya Pasaka, na kipindi cha Noeli ni tarehe 26 Desemba au siku nyingine yoyote ifaayo. 

KITUBIO (UPATANISHO)
Parokia Teule ya Mt. Moca Langoni inatoa Huduma ya kitubio kwa waamini wake kila siku za juma mara baada ya Misa za kazi asubuhi. Pia huduma hii hutolewa Jumuiyani kabla ya adhimisho la Misa Takatifu.
Siku ya Jumamosi ni mahususi ya kitubio kwa watoto na na wanafunzi. 
Parokia inawahimiza waamini wote kuzitumia siku hizi vizuri katika kujiweka karibu na Mungu wakati wote.

MPAKO WA WAGONJWA
Parokia Teule ya Mt. Monica Inao Utaratibu wa kutoa Huduma hii kwa wagonjwa wa majumbani wakati wa Pasaka, wakati wa Misa za Jumuiya katikati ya juma na wakati wowote huduma ya dharura itakapo jitokeza.Na kwa kushirikia na viongozi wa JNNK zote na kanda wameweka utaribu wa kuwasiliana kila mara pale mgonjwa wa jumuiya husika anapoomba ama kuhitaji huduma hii. Sakramenti hii siyo tu kwa wale walio katika hatari ya kufa bali hata walio katika hali ya ugonjwa na uzee pia.